MKASA::::::MAPENZI SI UTAJIRI
Kisa chenye mazingatio Jamaa mmoja Alimpenda mno mke wake, alijitahidi kumpa mkewe kila kitu kilochopo ndani ya uwezo wake, lakini mke wake hakuwa akiridhika na ku appriciate. Ingawa hakuwa tajiri lakini alijitahidi mno ku share kile alichonacho. Kila alipomnunulia nguo mkewe, jibu pekee alilolipata lilikuwa ni kwamba alikuwa akikamilisha jukumu lake kama mume. Mkewe hakuwahi kutoa shukrani hata mara moja. Mwanaume angemnunulia nguo mkewe lakini mkewe alikuwa akimjibu kwamba nguo ni ya bei ya chini na quality yake ni ndogo. Mume angetabasamu na kumwambia mkewe kwamba "siku moja nitakapokuwa tajiri nitakununulia vitu vyote vya gharama unavyovitaka" kwa sasa naomba nivumilie tu mke wangu! Mke hakuwa akimpigia simu mume wake labda tu pale alipokuwa akihitaji kitu au pesa kutoka kwa mumewe, na kama asipokamilishiwa ombi lake ilikuwa ni ugomvi kwa siku kadhaa. Jioni moja, mume alirudi kutoka kazini, alileta nyumbani kilogramu moja ya nyama, kwa furaha tele alitegemea k...